Episodes

Friday Jan 01, 2021
Tafakari Njia Yako
Friday Jan 01, 2021
Friday Jan 01, 2021
Heri ya Mwaka Mpya! Siku za kwanza za mwaka mpya ni wakati mzuri wa kutathmini juu ya maisha yetu, huduma yetu, na hali yetu ya kiroho kama viongozi. Podcast hii ni ujumbe maalum nilioandaa kwa ajili yako tunapoanza mwaka 2021. Kama umeanza kuchoka, kushuka moyo, au kukosa maono katika huduma, naomba usikilize podcast hii na kutiwa moyo. Tutaangalia mfano wa watu wa Mungu waliochoka na kupoteza furaha katika huduma, lakini kupitia ujumbe wa nabii wa Mungu walisaidiwa sana na hatimaye kuona mafanikio, ridhaa, na furaha katika huduma yao mbele za Bwana.

Monday Nov 30, 2020
Kiongozi na Timu Yake 2
Monday Nov 30, 2020
Monday Nov 30, 2020
Si watu wote wanaofaa kufanya huduma katika timu. Kiongozi lazima awe na tabia fulani na wanatimu pia wawe watu wa namna ya pekee. Sikiliza podcast hii tunapoendelea na mada ya "timu" na kuzungumzia ubora wa kufanya huduma pamoja na watu wengine wanaofaa.

Sunday Nov 15, 2020
Kiongozi na Timu Yake 1
Sunday Nov 15, 2020
Sunday Nov 15, 2020
Mhubiri alisema, "Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; kwa sababu wana tuzo njema kwa kazi yao." (Mhubiri 4:9). Katika podcast hii na podcast ijayo tutasikia kutoka kwa kiongozi wa kiroho ambaye amekuwa akiongoza timu katika huduma siku nyingi, katika mahali ambapo ardhi ni ngumu na nguvu ya timu ni muhimu. Anatushauri namna gani tunaweza kuwekeza katika watu wengine na kuona manufaa na matunda kwa kufanya huduma pamoja.

Friday Oct 30, 2020
Kuishi Kama Mfu
Friday Oct 30, 2020
Friday Oct 30, 2020
Sisi tulio viongozi wa kiroho mara nyingi huathiriwa na sauti za watu waliotuzunguka. Sauti za sifa, na sauti za malalamiko hufuatana na kiongozi yeyote siku zote. Lakini Biblia inasema nini juu ya sauti zile? Kama wafuasi wa Yesu Kristo, sisi tunapaswa kuishi kama watu waliosulibiwa. Kwa maneno mengine, tumtegee Mungu sikio letu na kutosikiliza sana sauti za watu aidha wanapotusifu au wanapolalamika juu yetu.

Thursday Oct 15, 2020
Kufikia Vijana Wasiookoka
Thursday Oct 15, 2020
Thursday Oct 15, 2020
Katika podcast hii ya tatu tunamaliza mkazo wetu juu ya Huduma ya Vijana na kusikia kutoka kwa Ndugu Abraham Stanslaus kuhusu kuwafikia vijana wasiookoka. Haitoshi kuandaa huduma nzuri kanisani na kukaribisha vijana. Ni juu yetu kutafuta vijana wanaohitaji habari njema na kuwapelekea Injili popote walipo. Kwa njia gani? Kiongozi huyu anatushirikisha vile wanavyofanya kanisani kwao.

Wednesday Sep 30, 2020
Kwa Njia Gani Tulenge Vijana?
Wednesday Sep 30, 2020
Wednesday Sep 30, 2020
Tumeisha ona kwamba tusipolenga vijana na kuwafikia na Injili tutapoteza nafasi ya kufikia kizazi kijacho na kushindwa kuona mafanikio kanisani. Vijana ni muhimu. Lakini vijana wana mahitaji ya pekee na kuna majaribio mengi sana yanayowavuta siku hizi. Kwa njia gani tunaweza kuwahudumia na kuwafikia kama viongozi kanisani? Katika podcast ya leo na ijayo tutapata mashauri kutoka kwa Mchungaji Abraham Stanslaus na tutaendelea kuhimizwa kuwalenga vijana katika huduma zetu.

Tuesday Sep 15, 2020
Kwa Nini Tulenge Vijana?
Tuesday Sep 15, 2020
Tuesday Sep 15, 2020
Tusipolenga kuwafikia vijana, tutapoteza kizazi cha sasa, tutakosa nguvu katika huduma, na tutashindwa kuendeleza Injili popote tulipo. Katika podcast hii tunazungumza na mtu ambaye ana moyo wa kuhudumia vijana na amefanya huduma ya vijana kwa mafanikio ya juu kwa siku nyingi. Sikiliza anapoeleza umuhimu wa huduma ya vijana na kutusihi kuwalenga vijana katika huduma zetu ndani na nje ya kanisa.

Sunday Aug 30, 2020
Tuwe Radhi Kuumizaana
Sunday Aug 30, 2020
Sunday Aug 30, 2020
Kila Kiongozi wa Kiroho anahitaji watu wa namna mbili katika maisha yake. Anahitaji maadui wanaosema ukweli na anahitaji marafiki waaminifu wasemao ukweli. Na yeye kama kiongozi anapaswa kuwa tayari kusema ukweli na watu wengine hata ingawa maneno yake yatawaumiza. Ndiyo maana ya podcast hii, kwamba tuwe tayari kuumizaana kwa kusema maneno ya ukweli na kufanya kwa upendo.

Saturday Aug 15, 2020
Familia ya Kiongozi: Utunzaji wa Familia
Saturday Aug 15, 2020
Saturday Aug 15, 2020
Kwa njia gani kiongozi anaweza kutunza familia yake ili wawe na furaha na amani nyumbani na kuwa baraka na msaada katika huduma badala ya mzigo? Katika podcast hii tunaendelea na maongezi yetu na Mchungaji Onesimus Kibera juu ya familia ya kiongozi wa kiroho. Anatupa mashauri mazuri juu ya familia na namna gani kiongozi anaweza kuwaongoza familia ili wamfuate Bwana kwa pamoja na kwa moyo.

Thursday Jul 30, 2020
Familia ya Kiongozi: Umuhimu wa Familia
Thursday Jul 30, 2020
Thursday Jul 30, 2020
Pasipo familia yenye ushuhuda mzuri na sifa njema, kiongozi atakosa nguvu na msaada unaotakiwa katika huduma yake. Mchungaji Onesimus Kibera anashiriki nasi katika podcast hii akieleza umuhimu wa familia katika maisha na huduma ya kiongozi wa kiroho.