The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kanuni Muhimu - Seh. 1

Kanuni Muhimu - Seh. 1

December 3, 2022

Sisi sote tuna mawazo yetu juu ya kanisa na uongozi katika kanisa, lakini mawazo yetu siyo sawa. Ni kwa sababu tumeathiriwa na mila na utamaduni pamoja na uzoefu wetu tangu utoto. Kuna aina mbalimbali za makanisa na namna tofauti tofauti za uongozi katika kanisa. Je, zote zinakubalika? Zote ni za kibiblia? Podcast hii na zingine zifuatazo zitahusu mada hii ya kanuni muhimu kutoka Neno la Mungu zinazotuongoza tuwe na kanisa la kibiblia na uongozi unaokubaliwa na Bwana.

Kulea Viongozi Wengine

Kulea Viongozi Wengine

October 15, 2022

Mzee Smith anazungumza na mchungaji ambaye, pamoja na kuongoza kanisa na kufanya huduma nyingine nyingi, anaweka mkazo katika kazi muhimu ya kulea viongozi wengine. Sikiliza mashauri yake namna ya kutambua viongozi wa siku zijazo na jinsi ambavyo mchungaji anaweza kuwafundisha na kuwalea katika kanisa.

Mauti Imemezwa

Mauti Imemezwa

August 11, 2022

Tunapoomboleza kifo cha ndugu zetu, viongozi wenzetu, hebu tukumbuke mambo haya.

Uzazi Bora

Uzazi Bora

June 2, 2022

Tuko na mkurugenzi wa Huruma Children’s Home katika podcast ya leo. Mzee Smith alikaa naye ili kumhoji juu ya ulezi wa watoto na vile ambavyo tunaweza kuwa wazazi bora katika ulezi wetu wa watoto. Usikose podcast hii ambayo imejaa hekima na mashauri mazuri kwa ajili yetu sisi tulio wazazi.

Mafunzo Jangwani, Seh. ya 2

Mafunzo Jangwani, Seh. ya 2

May 4, 2022

Katika podcast hii tunaendelea kujifunza kutoka kwa mfano wa Musa aliyepelekwa na Bwana jangwani kwa ajili ya mafunzo. Wakati ulipowadia atoke jangwani na kuingia katika huduma alikataa, akiona hawezi. Pengine wewe unatoa udhuru kama Musa. Tuone Mungu anasemaje juu ya kiongozi aliyeweza kutumiwa naye kutenda makuu.

Mafunzo Jangwani, Seh. ya 1

Mafunzo Jangwani, Seh. ya 1

April 6, 2022

Je, kiongozi mkuu ni yule ambaye ni mnenanji mzuri, ana talanta na vipaji vya pekee, na anasifiwa na watu? La, hasha. Katika mfano wa Mtumishi Musa tunaona kwamba mara nyingi ni kinyume. Kiongozi mkuu ambaye Mungu hupenda kumtumia ni yule ambaye amepita katika jangwa na kujifunza kuwa mwaminifu katika madogo, akimtegemea Bwana kwa unyenyekevu.

Awamu Mpya

Awamu Mpya

March 4, 2022

Tunamkaribisha Mzee Vernon Smith ambaye anajiunga na huduma ya podcast ya Uongozi wa Kiroho na atakuwa akichangia podcast mara kwa mara.

Agizo Kuu na Wajibu Wetu

Agizo Kuu na Wajibu Wetu

January 28, 2022

Wajibu wa kila mwamini na kila kanisa ni kutii Agizo Kuu la Yesu. Lakini kweli inawezekana katika mahali ambapo kanisa ni maskini kiuchumi na vikwazo ni vingi? Kwa njia gani mtu anayesikia wito wa kupeleka Injili kwa wasiowahi kusikia Habari Njema anaweza kujiandaa na kuenda? Maswali kama hayo ni mada ya podcast hii tunapoendelea na mahojiano na Dr. Richard Lewis.

Agizo Kuu na Kanisa la Afrika

Agizo Kuu na Kanisa la Afrika

December 30, 2021

Dr. Richard Lewis anaeleza vile ambavyo mustakabali wa huduma ya umisionari umo mikononi mwa kanisa la Marekani ya Kusini, Asia na Afrika na anatoa changamoto kwa ajili ya wasikilizaji wa podcast tuwe tayari kujibu wito wa Bwana pasipo hofu na kuongoza makanisa yetu kufundisha, kutuma na kusapoti wamisionari wanaopeleka injili kwa watu wasiowahi kusikia habari njema ya wokovu katika Yesu.

Sifa za Kiongozi 4 - Msingi Wako

Sifa za Kiongozi 4 - Msingi Wako

November 27, 2021

Inawezekana kiongozi wa mambo ya kiroho asisome Neno la Mungu kwa uaminifu? Ndiyo. Katika podcast hii kuna mashauri na mapendekezo kwa ajili ya kiongozi wa kiroho ambaye ana moyo wa kujenga maisha na huduma yake juu ya msingi ulio bora.

Podbean App

Play this podcast on Podbean App