Episodes

Friday Jan 28, 2022
Agizo Kuu na Wajibu Wetu
Friday Jan 28, 2022
Friday Jan 28, 2022
Wajibu wa kila mwamini na kila kanisa ni kutii Agizo Kuu la Yesu. Lakini kweli inawezekana katika mahali ambapo kanisa ni maskini kiuchumi na vikwazo ni vingi? Kwa njia gani mtu anayesikia wito wa kupeleka Injili kwa wasiowahi kusikia Habari Njema anaweza kujiandaa na kuenda? Maswali kama hayo ni mada ya podcast hii tunapoendelea na mahojiano na Dr. Richard Lewis.

Thursday Dec 30, 2021
Agizo Kuu na Kanisa la Afrika
Thursday Dec 30, 2021
Thursday Dec 30, 2021
Dr. Richard Lewis anaeleza vile ambavyo mustakabali wa huduma ya umisionari umo mikononi mwa kanisa la Marekani ya Kusini, Asia na Afrika na anatoa changamoto kwa ajili ya wasikilizaji wa podcast tuwe tayari kujibu wito wa Bwana pasipo hofu na kuongoza makanisa yetu kufundisha, kutuma na kusapoti wamisionari wanaopeleka injili kwa watu wasiowahi kusikia habari njema ya wokovu katika Yesu.

Saturday Nov 27, 2021
Sifa za Kiongozi 4 - Msingi Wako
Saturday Nov 27, 2021
Saturday Nov 27, 2021
Inawezekana kiongozi wa mambo ya kiroho asisome Neno la Mungu kwa uaminifu? Ndiyo. Katika podcast hii kuna mashauri na mapendekezo kwa ajili ya kiongozi wa kiroho ambaye ana moyo wa kujenga maisha na huduma yake juu ya msingi ulio bora.

Wednesday Oct 27, 2021
Sifa za Kiongozi 3 - Fedha ya Aibu
Wednesday Oct 27, 2021
Wednesday Oct 27, 2021
Kila kiongozi wa kiroho anapaswa kujiuliza swali: “Kwa nini ninamtumikia Bwana?” Amini, usiamini, kuna viongozi wengi ambao wamesahau wito wao na maana yake na wameanza kufanya huduma kwa ajili ya mapato. Katika podcast hii tutaangalia Neno la Mungu kwa viongozi kupitia waraka wa Paulo kwa Timotheo. Je, unatamani fedha ya aibu?

Thursday Sep 02, 2021
Sifa za Kiongozi 2 - Kauli Moja
Thursday Sep 02, 2021
Thursday Sep 02, 2021
Katika podcast hii tunaendelea kukazia sifa muhimu za Kiongozi wa Kiroho. Lazima atawale ulimi wake na kutunza maneno yake na asiwe mtu wa kusengenya watu. Kiongozi awe mtu anayesema wazi, bila kuficha ficha maana yake, na asiwe mtu wa kuwasema watu wengine.

Monday Aug 02, 2021
Maisha ya Umisionari
Monday Aug 02, 2021
Monday Aug 02, 2021
Mmisionari ambaye amekubali wito wa Bwana na kutumwa kwa watu wa lugha na utamaduni tofauti hupaswa kuzoea maisha mapya. Kuna changamoto nyingi, lakini pia kuna baraka kwa sababu ya kutii sauti ya Bwana na kumtegemea Yeye aliyemwita. Katika podcast hii tunaendelea na maongezi yetu na Mmisionari Daudi Likama na kusikia ushuhuda wake juu ya maisha na huduma yake Msumbiji. Bwana atumie ushuhuda wake ili kutuhimiza sisi sote na kufanya masikio yetu tayari kusikia wito wa Bwana kwa ajili yetu.

Friday Jul 02, 2021
Kuitikia Wito wa Umisionari
Friday Jul 02, 2021
Friday Jul 02, 2021
Wengi walisema “haiwezekani!” Walidai kwamba Tanzania ni nchi maskini na kuna haja ya wamisionari kuja Tanzania na kuleta Injili. Lakini Mmisionari Mtanzania kutumwa na kanisa la Tanzania na kupeleka Injili nje si rahisi. Lakini Bwana aliita na Ndugu Likama aliitika. Jiunga nasi katika podcast hii na ijayo ili kusikia ushuhuda wa Ndugu Daudi Likama aliyetumwa na kanisa lake kupeleka habari njema ya wokovu Msumbiji.

Monday Feb 15, 2021
Sifa za Kiongozi 1- Msimamo
Monday Feb 15, 2021
Monday Feb 15, 2021
Walio viongozi kweli kweli si viongozi wa jina tu, bali ni viongozi waliostahili kuongoza kutokana na msimamo wao na uaminifu wao mbele za Mungu na mbele ya watu. Katika podcast hii ya na podcast zifuatazo tutaangalia sifa za muhimu ambazo humfanya mtu awe kiongozi mwaminifu aliyetumiwa na Bwana kuongoza wengine vema.

Saturday Jan 30, 2021
Hekima Kutoka Kwa Kiongozi Mwanamke
Saturday Jan 30, 2021
Saturday Jan 30, 2021
Sikiliza mashauri na hekima ya mwanamke mwaminifu ambaye amekuwa kiongozi wa kiroho siku nyingi. Katika podcast hii tunamwuliza juu ya familia yake, huduma yake, baraka na changamoto anazoziona katika uongozi wake n.k. Podcast hii si tu kwa ajili ya akina dada. Kiongozi mwanamume, sisi pia tunahitaji hekima hii kutoka kwa Mama Moses. Karibu tusikilize!

Friday Jan 15, 2021
Ubora wa Viongozi Wanawake
Friday Jan 15, 2021
Friday Jan 15, 2021
Je, ni lazima mwanamke awe nyuma ya mwanamume katika ulimwengu wa uongozi? Wanawake wanafaa tu kusaidia waume zao na wanaume wengine, au wanawake wanafaa kuongoza wenyewe katika mambo ya kiroho? Katika podcast hii tunaongea na wanawake waaminifu walio viongozi wenyewe. Ni wake wa wachungaji na wasaidizi wa waume zao katika huduma. Lakini hawa wanawake ni zaidi ya wasaidizi. Wenyewe wanaongoza katika huduma na wao wenyewe ni viongozi katika mambo ya kiroho.